Ndoa ni kitu chema ambacho Mwenyezi Mungu amekiweka ili kila
binadamu aishi katika utukufu hapa duniani,maandiko Matakatifu yanatueleza kuwa
Mungu alipomuumba Adam aliona sio vyema Adam aishi peke yake,ndipo Mungu akamuumba
Hawa, ili asaidiane Adamu na waweze kuzaliana ili waijaze Dunia.
Ndoa zimekuwa chanzo za mafanikio na furaha katika maisha ya
watu na wengine imekuwa ndo chanzo cha maanguko
na majonzi katika maisha yao.
Leo tunangalia jinsi ndoa imetumika kwa baadhi ya watu
katika kufikia mafanikio na malengo yao, tuanze kwa kuangalia mafanikio
yaliyopatikana kwa baadhi ya watu ili wewe ujipime na kuona umefanikiwa kwa
kiwango gani au ndoa iwe ndo chanzo cha mafanikio kwenye malengo yako, tuanze kwa
kuangalia yafuatayo.
1. Kutakatifuzana.
Mwenyezi Mungu aliiweka ndoa ili wanandoa
wafundishane na kuelekezana njia ile impendezayo, wanandoa wengi wamekuwa
wakionyana pale mmoja wapo anapokuwa na tabia isiyompendeza Mungu na jamii kwa ujumla
mfano Mwanaume au Mwanamke anapokuwa mlevi wa kupindukia, mgomvi, kutukana
hovyo, uhuni na tabia nyingine zinazoikera jamii, wanandoa wengi wamekuwa
wakionyana, hali inayomfanya mtu atende mambo yaliyo mema na yanayo Mpendeza
Mungu, na mwisho wa ndoa yao hapa duniani wakutane Mbinguni.
2.Kushauriana
na kuongozana.
Kuna
baadhi ya wanaume na wanawake wamefanikiwa sana na kuwa viongozi wakubwa,
kutokana na ushauri wanaoupata kwa wenzi wao, wanawake wengi wamekuwa
wakiwashauri waume zao kwenye njia bora ya maisha, hali iliyowafanya wawe
matajiri wakubwa duniani, na wengine kuwa viongozi wakubwa, kuna ule msemo wa
kizungu usemao “ In any success of a man, there is a woman behind, and in any
success of a woman, there is a man behind” Nilazima utambue wapo watu wengi
wamefanikiwa kuingia kwenye ndoa, na wapo wengi walioaribikiwa na kupoteza dira
ya maisha kwa kuingia kwenye ndoa, kuwa makini tizama malengo yako, na ujiulize
unayetaka kuishi nae atakuwa msaada kwako? Au atakuwa kikwazo kwenye mipango
yako?
Zingatia haya, Usijaribu kumlazimisha
mtu akupende, afanye kama unavyofanya wewe au aishi na wewe, tambua mtu
anayekutenga au anayejaribu kuwa mbali nawe, anayekuchukia au asiyependa mambo
yako, huku wewe ukiamini ufanyayo ni mema kwa Mungu na jamii, usihofu kwani wewe ni mwenye bahati, kwani
kama huyo anayekukimbia angeungana nawe dhahiri angekuwa kikwazo kwako.
Wapo
watu wengi wanavutiwa na mipango na maisha yako, akupendae hawezi kukutenga,
hata ukifanya kosa atakuwa karibu nawe na atakushauri kuhusu mambo yaliyo mema,
tulia mwombe Mungu, fanya maamuzi sahihi, ndoa iwe chanzo cha mafanikio yako.
3. Malezi
ya watoto.
Kwa
ndoa zilizobahatika kupata watoto ndoa zimekuwa chanzo cha malezi ya watoto,
watoto ambao wameweza kuwa Viongozi wazuri, Wafanyakazi wazuri na watu wenye
mchango na msaada mkubwa kwenye jamii, kwa watu wenye tabia zisizopendwa na
jamii asilimia kubwa ya tabia zao zimetokana na malezi mabovu ya kuyumba kwa
ndoa au waliokosa malezi bora ya wazazi, ila tambua ndoa zimekuwa chanzo cha
mafanikio kwa malezi ya watoto.
4.Ushirikiano
Ndoa imekuwa ni sehemu ya kwanza kwa kuleta ushirikiano hasa kwa
wanandoa, wanandoa wamekuwa wakishirikiana ili kukuza kipato cha familia, mfano
Baba au mama inawezekana akawa ameajiriwa au amejiajiri ili kuepuka utegemezi
kwenye ndoa kwani mizani ya kipato ikiwa imeegemea upande mmoja, inawezekana
ndoa ikakosa furaha na amani kwani mmoja ya wanandoa atakuwa omba omba kwenye
ndoa yake na wakati mwingine yawezekana asipate anachoomba, kwa kutambua hilo
wanandoa wamekuwa na biashara za kuiendeleza familia kama hawakupata bahati ya
kuajiriwa, hii imekuwa msaada tosha kwani yawezatokea mmoja wao akakwama
kibiashara, kwenye ajira za kuajiriwa au kiafya, mmoja ya wanandoa akaweza kuendeleza
kazi na hatimae kufikia malengo.
Hitimisho.
Kufikia malengo katika maisha, ushirikiano
unahitajika, ndani ya ndoa au nje ya ndoa, ila unapokuwa na malengo kwenye
maisha yako ikiwa ni kupata mali au ndoa bora yote haya yahitaji kumwomba
Mungu, Kwani kila ukipatacho kwa kumwomba Mungu huwa kitamu na tena kizuri,
wengi waliofanikiwa maishani kwa kutumia ndoa zao, Mungu amekuwa ndo msaada kwao,
haijalishi Imani za kidini, Mwombe Mungu kwa Roho yako na sii kwa dini yako, Wapo
Wakristo, Waislamu wanamwomba Mungu kwa dini zao, lakini ukienda magerezani hawa
ndo wengi waliofungwa huko, ila wazee wetu walimwomba Mungu wakiwa hawana dini ila
mvua, chakula, ndoa nzuri, watoto, mali, walipata, Ndani ya MUNGU kuna raha sana, asante.
Mungu akubariki.