14 Sep 2016

TUMIA NDOA YAKO KUFIKIA MALENGO YAKO


Ndoa ni kitu chema ambacho Mwenyezi Mungu amekiweka ili kila binadamu aishi katika utukufu hapa duniani,maandiko Matakatifu yanatueleza kuwa Mungu alipomuumba Adam aliona sio vyema Adam aishi peke yake,ndipo Mungu akamuumba Hawa, ili asaidiane Adamu na waweze kuzaliana ili waijaze Dunia.
Ndoa zimekuwa chanzo za mafanikio na furaha katika maisha ya watu na wengine imekuwa ndo  chanzo cha maanguko na majonzi katika maisha yao.
Leo tunangalia jinsi ndoa imetumika kwa baadhi ya watu katika kufikia mafanikio na malengo yao, tuanze kwa kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwa baadhi ya watu ili wewe ujipime na kuona umefanikiwa kwa kiwango gani au ndoa iwe ndo chanzo cha mafanikio kwenye malengo yako, tuanze kwa kuangalia yafuatayo.
1.       Kutakatifuzana.
Mwenyezi Mungu aliiweka ndoa ili wanandoa wafundishane na kuelekezana njia ile impendezayo, wanandoa wengi wamekuwa wakionyana pale mmoja wapo anapokuwa na tabia isiyompendeza Mungu na jamii kwa ujumla mfano Mwanaume au Mwanamke anapokuwa mlevi wa kupindukia, mgomvi, kutukana hovyo, uhuni na tabia nyingine zinazoikera jamii, wanandoa wengi wamekuwa wakionyana, hali inayomfanya mtu atende mambo yaliyo mema na yanayo Mpendeza Mungu, na mwisho wa ndoa yao hapa duniani wakutane Mbinguni.

2.Kushauriana na kuongozana.
 Kuna baadhi ya wanaume na wanawake wamefanikiwa sana na kuwa viongozi wakubwa, kutokana na ushauri wanaoupata kwa wenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakiwashauri waume zao kwenye njia bora ya maisha, hali iliyowafanya wawe matajiri wakubwa duniani, na wengine kuwa viongozi wakubwa, kuna ule msemo wa kizungu usemao “ In any success of a man, there is a woman behind, and in any success of a woman, there is a man behind” Nilazima utambue wapo watu wengi wamefanikiwa kuingia kwenye ndoa, na wapo wengi walioaribikiwa na kupoteza dira ya maisha kwa kuingia kwenye ndoa, kuwa makini tizama malengo yako, na ujiulize unayetaka kuishi nae atakuwa msaada kwako? Au atakuwa kikwazo kwenye mipango yako?
 Zingatia haya, Usijaribu kumlazimisha mtu akupende, afanye kama unavyofanya wewe au aishi na wewe, tambua mtu anayekutenga au anayejaribu kuwa mbali nawe, anayekuchukia au asiyependa mambo yako, huku wewe ukiamini ufanyayo ni mema kwa Mungu na  jamii, usihofu kwani wewe ni mwenye bahati, kwani kama huyo anayekukimbia angeungana nawe dhahiri angekuwa kikwazo kwako.
 Wapo watu wengi wanavutiwa na mipango na maisha yako, akupendae hawezi kukutenga, hata ukifanya kosa atakuwa karibu nawe na atakushauri kuhusu mambo yaliyo mema, tulia mwombe Mungu, fanya maamuzi sahihi, ndoa iwe chanzo cha mafanikio yako.

3. Malezi ya watoto.
  Kwa ndoa zilizobahatika kupata watoto ndoa zimekuwa chanzo cha malezi ya watoto, watoto ambao wameweza kuwa Viongozi wazuri, Wafanyakazi wazuri na watu wenye mchango na msaada mkubwa kwenye jamii, kwa watu wenye tabia zisizopendwa na jamii asilimia kubwa ya tabia zao zimetokana na malezi mabovu ya kuyumba kwa ndoa au waliokosa malezi bora ya wazazi, ila tambua ndoa zimekuwa chanzo cha mafanikio kwa malezi ya watoto.


4.Ushirikiano

   Ndoa imekuwa ni sehemu ya kwanza kwa kuleta ushirikiano hasa kwa wanandoa, wanandoa wamekuwa wakishirikiana ili kukuza kipato cha familia, mfano Baba au mama inawezekana akawa ameajiriwa au amejiajiri ili kuepuka utegemezi kwenye ndoa kwani mizani ya kipato ikiwa imeegemea upande mmoja, inawezekana ndoa ikakosa furaha na amani kwani mmoja ya wanandoa atakuwa omba omba kwenye ndoa yake na wakati mwingine yawezekana asipate anachoomba, kwa kutambua hilo wanandoa wamekuwa na biashara za kuiendeleza familia kama hawakupata bahati ya kuajiriwa, hii imekuwa msaada tosha kwani yawezatokea mmoja wao akakwama kibiashara, kwenye ajira za kuajiriwa au kiafya, mmoja ya wanandoa akaweza kuendeleza kazi na hatimae kufikia malengo.

Hitimisho.
Kufikia malengo katika maisha, ushirikiano unahitajika, ndani ya ndoa au nje ya ndoa, ila unapokuwa na malengo kwenye maisha yako ikiwa ni kupata mali au ndoa bora yote haya yahitaji kumwomba Mungu, Kwani kila ukipatacho kwa kumwomba Mungu huwa kitamu na tena kizuri, wengi waliofanikiwa maishani kwa kutumia ndoa zao, Mungu amekuwa ndo msaada kwao, haijalishi Imani za kidini, Mwombe Mungu kwa Roho yako na sii kwa dini yako, Wapo Wakristo, Waislamu wanamwomba Mungu kwa dini zao, lakini ukienda magerezani hawa ndo wengi waliofungwa huko, ila wazee wetu walimwomba Mungu wakiwa hawana dini ila mvua, chakula, ndoa nzuri, watoto, mali, walipata, Ndani ya MUNGU kuna raha sana, asante.
 Mungu akubariki.




0 maoni:

Chapisha Maoni