Utangulizi.
Tanzania ni moja ya nchi zilizobarikiwa sana na Mwenyezi
Mungu Kuwa na fursa mbalimbali za maendeleo kulingana na Jeografia ya nchi
yetu, fursa ambazo zimetumika na baadhi ya watanzania na wawekezaji kutoka nje
ya Nchi kujipatia maendeleo na kuwa matajiri wakubwa.
Katika nchi yetu
Tanzania kila mkoa umebarikiwa kuwa na fursa mbalimbali za maendeleo ikawa ni
pamoja na vivutio vya utalii vinavyotumiwa na wananchi pamoja na serikali
kujipatia mapato.
Kwa Jiji kama Dar
es salaam, limekuwa likitumiwa kwa shughuli nyingi za Kiserikali, ikiwa ni
pamoja na Ofisi nyigi za wizara mbalimbali kuwa kwenye Jiji hilo, pamoja na
hilo, Jiji hilo limekuwa ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika mashariki na
kusini mwa Afrika kutokana na mazingira lililopo jiji hilo kwani limepakana na bandari ya Dar es salaam
inayotumika kuingiza mizigo na bidhaa nyingi
kutoka nje ya nchi, bidhaa zinazo tumika ndani na nje ya Tanzania kwa
nchi kama Uganda, Jamuhuri ya Kimokrasia ya Kongo, Zambia, Malawi, Rwanda na
Burundi, hivyo watu wengi wamevutiwa kwenda kuwekeza kwenye Jiji hilo.
Serikali ya awamu ya tano kwa kukusudia imeamua kuamisha
shughuli za Serikali makao makuu kuwa katika mji wa Dodoma, hali ambayo imeleta
neema na fursa nyingi za maendeleo katika mji wa Dodoma….Tambua kuwa huu ndio
wakati wako, kama ulifika Dar es Salaam na kukukutana na mambo mengi
yaliyokushangaza, sasa ni wakati wako wa kufanya mambo makubwa na yakushanga ya
maendeleo katika mji wa Dodoma, nimekuandalia kitabu kinachoeleza fursa
mbalimbali za maendeleo zinazopatikana katika mji wa Dodoma na jinsi ya
kuwekeza kulingana na kipato chako, karibu twende pamoja
MIRADI YA MAENDELEO
1.Kuuza Tofali
Shughuli za ujenzi wa nyumba kwa ajili ya shughuli mbali mbali kwa mji wa Dodoma zitashika kasi sana, jinsi
ya kuwekeza kwenye shughuli za uuzaji wa tofali kutegemea na mtaji wako,
unaweza kufika Dodoma na ukanunua shamba, kiwanja au la ukaamua kukodi kiwanja kwa muda
utakaoona unakufaa kuwekeza na kupata mtaji wa kununua shamba au kiwanja chako
na kuanza kazi ya ufyatuaji wa tofali
2 Biashara ya Vyakula
Vyakula vitahitajika kwa kiwango kikubwa, jitahidi kuzalisha
au kufungua migahawa, hoteli au sehemu mbalimbali za kuuzia vyakula ili kuweza
kujipatia kipato.
3. Nyumba za kupangisha
Watu wengi watahamia Dodoma na watahitaji nyumba za kuishi na
wengine watahitaji nyumba kwaajili ya shughuli mbalimbali kama kufungulia ofisi.
4.Vifaa vya Maofisini
Maofisi mengi yatafunguliwa kwenye mji wa Dodoma, jitahidi
kufungua maduka au steshenari kwaaji ya kuuza vifaa vya maofisini.
5.Vyakula vya Mifugo
Kutokana na watu wengi kuhamia Dodoma, ufugaji wa kisasa
utastawi kwa kiasi kikubwa, mfano ufugaji wa ngombe wa kisasa, kuku wa nyama na
wa mayai, hivyo vyakula vya mifugo hiyo vitahitajika kwa kiwango kikubwa,
jitahidi kuchangamkia fursa hiyo kwa kujifunza kutengeneza au kununua na kuuza
vyakula hivyo.
6. Utengenezaji wa vinywaji
Dodoma ni Mkoa maarufu kwa kilimo cha Zabibu hapa Tanzania,
jitahidi kuchangamkia fursa ya kutengeneza Vinywaji kama Juisi au wine, na
makapi ya zabibu kutumika kwa shughuli mbalimbali kama kutengeneza mbolea kwaajili
ya mazao na vyakula vya mifugo.
Hitimisho
Hizo ni baadhi ya fursa zinazopatikana katika mji wa Dodoma,
kuna fursa nyingi sana ambazo sijaziorodhesha kwenye makala hii nakuomba
utembelee tovuti hii ya kijii.com ili uwezekupata mawazo mazuri ya maendeleo
yatayoweza kubadili maisha, Mungu akubariki sana, ahsante.
0 maoni:
Chapisha Maoni